Friday, August 3, 2018

Ujumbe wa twitter wa Sampdoria
Sampdoria yamzindua Ronaldo!
Hapana, sio uhamisho mkubwa wa msimu huu
Klabu hiyo ya Seria A imemsajili Ronaldo wao na kumpatia upinzani Christiano Ronaldo aliyeelekea klabu ya Juventus.
Haki miliki ya picha TwitterUjumbe wa twitter wa Sampdoria
Sampdoria yamzindua Ronaldo!
Image caption Hii ndio sababu unapaswa kusoma kwa makini
Ronaldo Vieira amejiunga na Blucerchiati kwa kandarasi ya miaka mitano , mkataba usiojulikana thamani yake kutoka klabu ya Leeds na anaweza kuanzishwa dhidi ya Fiorentina mnamo tarehe 19 Agosti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoka kikosi cha Uingereza cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka21 alitangazwa katika orodha ya wachezaji chipukizi wenye matumaini katika soka ya Ulaya mapema mwaka huu-hivyobasi haishangazi klabu yake mpya ilidhania anafaa kukaribishwa kwa mbwembwe kama Christiano Ronaldo.
Tangazo hilo lililofanywa katika akaunti ya twitter ya kiingereza ya klabu hiyo siku ya Ijumaa lilivutia majibu haya.
Haki miliki ya picha Twitter

0 comments:

Post a Comment