DAVID Molinga wengi
wanapenda kumuita mwili jumba ama falcao mshambuliaji wa Yanga raia wa
Congo guu lake la kulia limekwama uwanja wa CCM Kirumba kwa muda wa
dakika 270 bila kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara.
Molinga mwenye mabao
manne kwa sasa alianza kwa kasi ya kutupia huku akipata umaarufu kwa
kutumia zaidi guu la kulia kufunga mabao ya moja kwa moja akiwa nayo
mawili mpaka sasa akiwa.
Alianza kufunga bao
lake la kwanza kwenye mchezo wa pili wa Yanga dhidi ya Polisi Tanzania
kwenye sare ya mabao 3-3 ambapo alifunga dakika ya 64 kwa kichwa
akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa na la pili alifunga kwa faulo dakika
ya 68 kwa guu lake la kulia.
Bao la tatu alifunga
mbele ya JKT Tanzania kwa faulo dakika ya 34 baada ya Deus Kaseke
kuchezewa faulo na Yanga ilishinda mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania
mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
Mara ya mwisho
kufunga bao lake la nne ilikuwa uwanja wa CCM Kirumba ambapo guu lake la
kulia lilicheka na nyavu dakika 71 akimalizia pasi ya Deus Kaseke
kwenye ushindi wa mabao 2-1 na hakuweza kufurukuta kwenye mechi tatu za
Yanga ambazo ni sawa na dakika 270 akiwa uwanjani.

0 comments:
Post a Comment