Wakati tukisubiri uamuzi kutoka Uefa, wa kuondoa sheria ya goli la ugenini, acha nitoe mtazamo wangu.
Kuna mambo mawili yanayonishawishi ili goli la ugenini lisiondolewe. Goli la ugenini lina kimuhemuhe chake. Hili goli linatoa watu kijasho chembamba. Unalitoa vipi kwa mfano?
Jambo la kwanza ni mvuto wa mechi yenyewe.
Hivi ubakumbuka ule mchezo wa Buyern dhidi ya Man United Ferguson anamchezesha Rooney mgonjwa? Unakumbuka baada ya Roben kuoiga bao la pili alivyokuwa anashangilia kwa kung’ata kidole? Sasa wanataka kutuondolea ladha hii kwa sababu gani?
Wala tusiende mbali hivi majuzi tu tukumbuke mechi ya robo fainali ya Uefa, msimu uliopita kati ya Barcelona na As Roma, wengi tulisahau kama kuna mechi ya kwanza ilichezwa Nou Camp.
Kumbukumbu ilibaki katika uwanja wa Stadio Olimpico. Kitu pekee kilicholeta mvuto wa ile mechi ya robo fainali, ni lile goli tamu la ugenini lililofungwa na Roma, katika uwanja wa Nou Camp. Mechi ile iliisha kwa Barcelona kushinda 4-1
Barcelona walienda Stadio Olimpico, wakiwa tayari na matumaini makubwa ya kucheza nusu fainali. Ila kwasababu ya kile chakula cha ugenini ndo kilileta radha yenyewe. Hakuna kushuhudia timu ikipaki basi wakati inakumbuka ina deni. Mpaka unakosa usingizi kwa kuangalia mechi za mtoano.
Jambo la pili, ni kutambua ukomavu wa akili za wachezaji au mentality. Unapotambua kwamba unatakiwa urudishe magoli ili yalipe faraja goli la ugenini, basi lazima wachezaji wawe wanajitambua nini wanaenda kukifanya uwanjani.
Pia utaamini kweli wachezaji wa wana akili za kushinda mataji? Lazima uwe na wachezaji wanaojua nini maana ya mataji na sio vinginevyo. Uzoefu wa kushinda mataji utauona.
0 comments:
Post a Comment