Peter Manyika JR ang’atuka Singida United adai wamevunja mkataba
Mlindalango wa klabu ya Singida United, Peter Manyika JR amesema kuwa waajiri wake hao wamevunja mkataba baada ya kushindwa kumlipa mshahara kwa zaidi ya miezi mitatu, hivyo amejiondoa rasmi.
Mlindalango wa Singida United, Peter Manyika JR
Kwa mujibu wa kituo cha radio cha E FM, Manyika amesema kutokana na sababu hiyo sasa yeye ni mchezaji huru na anasubiri dirisha dogo aende kusaini timu nyingine aendelee na kazi.
Kwa sasa Manyika anafanya mazoezi kwenye kituo kinachosimamiwa na baba yake, Manyika ambaye pia ni kocha wa makipa wa timu za vijana za taifa.
0 comments:
Post a Comment