Saturday, September 1, 2018



Daktari wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Richard Yomba, amesema kuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula, yupo fiti kuanza mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Uganda.

Manula aliumia kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ambao Simba ilicheza dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuepelekea akose mazoezi ya Stars ambayo inajiandaa kucheza na Uganda, kuelekea kufuzu AFCON.

Yomba amesema hali ya Manula kwa sasa ipo sawa kwa yeye kuanza mazoezi na panapo majaliwa kesho Jumapili anaweza kuungana na wenzake kikosini.

Taarifa zinaeleza taayri Yomba ameshapata taarifa za daktari wa Manula, Yassin Gembe, ambaye ndiye daktari wa wachezaji Simba kuhusiana na ripoti ya majeruha yake tangu yampate kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Stars itakuwa inamenyana na Uganda Septemba 8 2018 huko Kampala ukiwa ni mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON.

0 comments:

Post a Comment