Klabu
tano kutoka Premier League zipo katika vita kubwa ya kuwania saini ya
mchezaji wa Barcelona, Philippe Coutinho katika msimu huu wa majira ya
joto na hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.
Kiungo
huyo wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anaitumikia Bayern Munich
inayoshiriki ligi ya Bundesliga kwa mkopo ameanza kuwa lulu kwa klabu
hizo za Uingereza.
Barcelona haina mpango tena na Coutinho baada
ya kushindwa kufanya makubwa kama yalivyotarajiwa na miamba hiyo ya soka
kutoka LaLiga baada ya kujiunga akitokea Anfield mwezi Januari mwaka
2018.
Akiwa
katika ukurasa wa mbele wa Deportivo hukukiwa na kichwa cha habari
kikubwa kilichoandikwa ‘Premier Coutinho’. Chelsea, Newcastle,
Manchester United, Arsenal na Leicester zote zimeonyesha nia ya kutaka
huduma ya Mbrazil huyo lakini klabu zote hizo zinadaiwa kutaka kutoa
kitita cha paundi milioni 90 ili kukamilisha dili hilo.
0 comments:
Post a Comment