Thursday, May 28, 2020


Mshambuliaji wa Nigeria, Odion Ighalo mwenye umri wa miaka 30,  ametuma maombi binafsi kwa klabu yake ya Shanghai Shenhua kumuacha arefushe mkataba wake wa mkopo ndani ya Manchester United ambao utamruhusu kuendelea kusalia hadi mwisho wa msimu kabla ya kurudi China.

Mkataba wake wa sasa wa mkopo utamalizika ndani ya Old Trafford siku ya Jumapili, huku mazungumzo baina ya United na washiriki hao wa Chinese Super League yamefeli baada ya kushindwa kuafikiana.
Hata hivyo, Odion Ighalo anatamani kuona anasalia United mpaka mwisho wa msimu hii ni baada ya kuwa na matokeo mazuri katika michezo yake nane aliyocheza hivyo na kuamua kuiomba Shanghai Shenhua kumruhusu asalie hapo Manchester hadi atakapomaliza msimu.

Shanghai Shenhua wanachohitaji wao ni kumuuza Ighalo moja kwa moja badala ya kusalia kwa mkopo, lakini kwa upande wa United wameweka wazi kuwa hawana mpango na usajili.
Malengo ya kocha, Ole Gunnar Solskjaer ni kuona mchezaji huyo anaongezewa muda wa mkopo baada ya kuingia United kwa mkopo wa miezi minne .

0 comments:

Post a Comment