Thursday, May 28, 2020


Kocha wa Borussia Dortmund, Lucien Favre ameungwa mkono na Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Hans-Joachim Watzke licha kipigo cha 1- 0 kutoka kwa Bayern Munich siku ya Jumanne.

“Nadhani Lucien amekuwa makini sana katika wiki zilizopita,” alisema Watzke. “Haonekani kama mtu anayekabiliwa na shinikizo,” aliongeza kusema.
Favre alisema baada ya kushindwa Jumanne angezungumza kuhusu hali ya Drtmund katika wiki chache zijazo, huku baadhi ya vyombo vya habari vikitafsiri kama dalili za uwezekano wa kuondoka kabla mkataba wake kukamilika 2021.
“Sifikirii kuhusu kukata tamaa. Nilichotaka kukisema ni kwamba huu sio wakati wa kufanya tathmini,” Favre aliliambia gazeti la WAZ siku ya Jumatano. “Tuna mechi sita kucheza na tunataka kufanya bidii kadri ya uwezo wetu.”
Bundesliga Borussia Dortmund v FC Bayern München Kimmich (Getty Images/F. Gambarini)
Ushindi wa bao 1-0 iliyoupata timu ya Bayern Munich dhidi ya timu ya Borussia Dortmund iliyoko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Bundesliga umewafanya vinara wa ligi hiyo Bayern Munich kuendelea kujikita kileleni kwa tofauti ya alama saba dhidi ya wapinzani wao wa karibu Borussia Dortmund.
Bayern Munich kwa hivi sasa ina matumaini ya kunyakua taji la nane la ligi kuu ya Bundesliga baada ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata Jumanne 26.05.2020, dhidi ya wapinzani wao wa karibu Borussia Dortmund.
Tofauti kati ya Bayern chini ya kocha wa zamani Niko Kovac na sasa chini ya Hansi Flick ilionekana katika mchezo mzuri na wa kujiamini katika ushindi wa bao 1-0, licha ya kutokuwepo na mashabiki uwanjani kulikosababishwa na kuzuka kwa mlipuko wa virusi vya Corona.

0 comments:

Post a Comment