Thursday, May 28, 2020



TIMO Werner, staa wa Klabu ya RB Leipzig raia wa Ujerumani amewekwa kwenye rada za vinara wa Ligi Kuu England Liverpool.


Werner mwenye miaka 24 anakipiga ndani ya RB Leipzig ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kwa jina la Bundesliga.


Anatajwa kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi akiwa ndani ya uwanja jambo linalowavutia mabosi wa timu nyingi.

Aliwahi kusema kuwa amefanya mazungumzo na Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp hivyo uwezekano wa kuibukia ndani ya Liverpool ni mkubwa.


 "Ninafahamu kuwa Liverpool ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri hivyo kama jina langu linatajwa pale nami ni mchezaji bora hivyo nami nimekuwa mkubwa,".

0 comments:

Post a Comment