Thursday, May 28, 2020



ANTONIO Nugaz,  Ofisa Muhamasishaji na Msemaji wa Yanga amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa msimu ujao wakashiriki michuano ya kimataifa kutokana na mipango waliyojiwekea.

 Nugaz amesema malengo yao ni kuhakikisha wanatwaa Kombe la Shirikisho, ambalo litawafungulia njia kurejea kwenye anga za kimataifa.

"Malengo yetu baada ya kurejea ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu zote ndani ya Kombe la FA na kuibuka mabingwa ambapo tutakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

"Hilo linawezekana kwani wachezaji wapo tayari na uongozi unatoa sapoti bega kwa bega kwa wachezaji, hivyo kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki ili kuona kwamba tunafikia malengo yetu," amesema.


Yanga ipo ndani ya timu nane ambazo zimetinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Azam FC.

0 comments:

Post a Comment