Tuesday, September 4, 2018



Katika hali isiyotarajiwa, mshindi mara 20 wa Grand Slam kutoka Uswisi Rodger Federer amejikuta nje ya michuano ya Us Open abaada ya kuondolewa na mchezaji namba 55 kwenye Tennis John Millman.

Kila mtu aliamini kwamba Federer vs Millman itakuwa mechi rahisi kwake lakini mashabiki waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya Flushing Meadows walishangazwa na matokeo ya mwisho.

Ushindi wa 3-6 7-5 7-6 7-6 katika muda wa masaa 3 na dakika 35 ulishuhudia Federer akiondolewa na huku hii ikiwa mara ya kwanza kwake kutolewa katika michuano mikubwa na mchezaji ambaye hayuko 50 bora.
Katika mechi 41 zilizopita za Federer hajawahi kufungwa na mchezaji aliyeko nje ya 50 ya juu, na Millman mwenyewe amekiri kutoamini alichofanya kutokana na heshima kubwa aliyonayo kwa Federer.

Katika mchezo mwingine Novack Djokovick naye amekwenda katika robo fainali baada ya kuibuka kidedea katika mechi yake dhidi ya Joao Sousa.
Djokovick ambaye ni bingwa mara mbili wa michuano hiyo alishinda mchezo huo kwa seti 6-3 6-4 na 6-3 na kwa ushindi huu sasa Djokovick anakwenda kukutana na John Millman

0 comments:

Post a Comment