Thursday, September 6, 2018

Kuelekea mchezo dhidi ya Uganda kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema lengo ni kufuzu fainali hizo kwa hiyo watu wasiangalie kushinda mechi dhidi ya Uganda pekee.
“Hii ni mechi ya majirani, hii sio mara ya kwanza tunacheza na Uganda na baadhi ya wachezaji tunawafahamu tumeshawahi kucheza nao kwa muda mrefu, haitokuwa mechi rahisi kwa sababu watu ambao mnafahamiana mnapokutana kwenye mechi inakuwa lakini tunajua mechi ina umuhimu gani.”
“Tunachokihitaji ni kufuzu kwenda AFCON kwa hiyo pamoja na mechi hii dhidi ya Uganda bado tunamechi nyingi ambazo zitakuwa ngumu vilevile kwa hiyo tuwaweke Uganda lakini lengo tunahitaji pointi ili tufuzu.”
Vipi kuhusu waliotemwa?
“Mwisho wa siku ni lazima tukubaliane na hali halisi, tunakwenda kwenye mchezo hakuna muda wa kuyazungumzia mambo ambayo hayawezi kutusaidia kwenye ule mchezo. Muhimu ni kuangalia kitu gani kitakachotusaidia kupata uhindi na wachezaji tulionao, nafikiri mwalimu anawaamini na kila mtu anatakiwa awaamini”-Mbwana Samatta, nahodha Taifa Stars.
Kwa hiyo tunaenda kupambana na mpinzani anaetufahamu na sisi tunamfamu, ni mchezo mbao utakuwa mgumu lakini mwisho wa siku tunahitaji ushindi hilo ndio kubwa. Mambo mengine tuachane nayo kwa sasa muhimu ni kupata ushindi katika mchezo wa Jumamosi.”

0 comments:

Post a Comment