Griezman awatolea “povu” FIFA na anaamini anastahili kushinda Ballon D’or
Kumekuwa na maneno mengi sana baada ya mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya nchini Ufaransa Antoine Griezman kutukuwepo kwenye orodha ya wanaogombania tuzo ya mchezaji bora UEFA.
Wachambuzi wengi wamepinga uamuzi huu wa FIFA na hadi mchambuzi nguli wa masuala ya michezo nchini Shaffih Dauda aliongea wazi kuonesha kutorodhishwa kwake na kukosekana kwa Griz au nyota yoyote wa Ufaransa.
Sasa wakati huu ambapo Griezman yuko kambini na timu ya taifa ya Ufaransa alifanikiwa kufanya mahojiano na jarida maarufu la nchini Ufaransa liitwalo L’Equipe.
Kwanza Griezman amekiri kwamba katika maisha yake ya soka, msimu wa ligi uliopita ndio ulikuwa msimu bora sana kwake katika uchezaji lakini vile vile katika kubeba makombe(Europa na kombe la dunia).
Kuhusu tuzo za FIFA “Ni aibu na inashangaza, hili kombe tumebeba si ndio kombe kubwa la FIFA na FIFA ndio wameandaaa tuzo? Sasa inakuwaje hatuna mchezaji hata mmoja?”
Griezman pia amefunguka kwamba anajiona anakaribia kushinda tuzo ya Ballon D’Or kila mwaka na mwaka huu asiposhinda itamshangaza ila ataona poa tu.
Griz anaamini mwaka 2016 hakupaswa kuwepo kwenye orodha ya washindani watatu wa mwisho lakini anaamini safari hii ana nafasi kubwa ya kuwepo katika wanaowania tuzo hiyo.
0 comments:
Post a Comment