Baada ya kuelezwa kusimamishwa kwa ratiba ya mchezo wa Simba dhidi ya African Lyon uliopaswa kuchezwa wikiendi hii, uongozi wa klabu hiyo umesema hakuna tatizo kwa mechi hiyo kupigwa.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema hawaoni tatizo kwa mechi hiyo kuchezwa kwani kuna uwekezekano wa ligi kumalizika nje ya muda.
Manara ameeleza kuwa TFF na Bodi ya ligi bado mpaka sasa hawajapeleka barua rasmi kwao inayoeleza kuwa wamesimamisha mchezo huo ambao inaelezwa utapangiwa tarehe nyingine.
Aidha, Manara amewashauri TFF kuangalia namna ratiba inavyokwenda ili kuja kuepuka ligi kutomalizika nje ya muda.
Ofisa huyo amesema huko mbele kuna ratiba nyingine zinakuja ikiwemo Mapinduzi CUP na Michuano ya Kimataifa hivyo ni vema wakaliangalia suala hili kwa jicho la tatu kuweka mambo sawa.
0 comments:
Post a Comment