Klabu ya soka ya AC Milan imepigwa adhabu ya mwaka mmoja ya kutoshiriki michuano ya Europa League msimu ujao.
AC
Milan iliyomaliza nafasi ya 5 kwenye ligi ya soka Italia, Serie A
imekumbana na kifungo hicho kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo
baada ya kuvunja sheria ya ‘Financial Fair Play’.
Kwa kifungo
hicho, nafasi ya AC Milan itachukuliwa moja kwa moja na AS Roma, Huku
Torino iliyomaliza katika nafasi ya 7 kwenye Ligi ya Serie A msimu
uliopita itaingia kwenye mechi za kufuzu ili kutinga hatua ya makundi.
Hata
hivyo adhabu hiyo imetoka baada ya AC Milan kufanikiwa kukata rufaa ya
kifungo cha miaka miwili, Wachopewa awali na UEFA msimu wa majira ya
joto uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria ya hiyo ya
‘Financial Fair Play’.
Home
»
»Unlabelled
» Klabu ya soka ya AC Milan yapigwa STOP kushiriki michuano ya Europa League barani Ulaya
Friday, June 28, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment