French football Professional Football League (LFP) imeeleza kuwa kampuni ya delivery ya chakula ya Uber Eats ndio wameshinda tenda ya udhamini wa kujitangaza kwa Ligi Kuu ya Ufaransa kuitwa kwa jina lao kutoka Ligue 1 hadi kuwa Ligue 1 Uber Eats.
Kwa mujibu wa gazeti la kifaransa la kila siku la Le Figaro linaeleza kuwa Uber Eats watailipa LFP kiasi cha pound milioni 28 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 81 ila inaweza kuongezeka kwa pound milioni 18 na zaidi, pia dili hilo litahusisha mpira wa game za Ligue 1 utaletwa na dereva wa Uber Eats kama delivery package kabla ya game kuanza.
0 comments:
Post a Comment