Monday, July 29, 2019


GARETH Bale bado yupoyupo ndani ya Real Madrid kutokana na uhamisho wake wa kujiunga na klabu tajiri ya China Jiangsu Suning kupotezewa.

Bale alikuwa anahitajika na klabu hiyo ya China ambayo ilipanga kumpa mshahara mkubwa kuliko timu ndani ya China.

 Bale alitarajiwa kujiunga na Jiangsu Suning kwa mshahara wa Pauni milioni moja ambazo ni sawa na Sh bilioni 2.8 za Tanzania.

Mabosi wa Real Madrid wamesitisha dili hilo kwa kuwa wanataka kulipwa fedha nyingi za uhamisho kwa nyota huyo ambaye kwa sasa hana maelewano mazuri na meneja wa Madrid, Zinadine Zidane.

0 comments:

Post a Comment