Thursday, August 1, 2019

BINGWA mara mbili wa Kombe la Mataifa Afrika, kocha Herve Renard, ametangazwa rasmi na Shirikisho la soka Saudi Arabia kuwa kocha mkuu kuelekea FIFA World Cup Qatar™ 2022.
Akiwa na kibarua cha kwanza kuitafutia nafasi ya mara ya sita kuirejesha Saudia arabia kwenye fainali hizo ambapo waliweza kushiriki mwaka 2018 huko Urusi.
Saudia Arabia au maarufu kwenye soka mwewe wa kijana, wapo kundi D dhidi ya
Uzbekistan, Palestine, Yemen na Singapore. 
Ambapo kinara wa kundi ataenda hatua  ya tatu kuungana na timu kumi na mbili.
Herve Renard amezipa ubingwa wa mataifa ya Afrika zambia na Ivory Coast, mwaka 2018 akiiongoza morocco kushiriki kombe la dunia baada ya miaka ishirini taifa hilo kukosa kushiriki kombe la dunia.

0 comments:

Post a Comment