Tuesday, August 27, 2019



NICOLAS Pepe, mshambuliaji wa kikosi cha Arsenal amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kumpiga chenga beki kisiki wa Liverpool, Virgil Van Dijk.

Mchezaji wa mwisho kufanya hivyo alikuwa ni kiungo wa Newcastle, Mikel Merino mwaka 2018.

Beki huyo kisiki alikuwa hajapitwa kwenye jumla ya mechi 50 zilizopita na amekuwa akitajwa miongoni mwa mabeki bora na ghali duniani.

Mchezo wake wa kwanza kuanza kwenye kikosi cha Arsenal kwa nyota huyu ambaye ana umri wa miaka 24 kwa sasa ulikuwa.

Licha ya kufanya maajabu hayo timu yake ilipoteza Kwa kuchapwa mabao 3-1 huku wafungaji wakiwa ni Mohamed Salah aliyetupia mawili na Joel Matip na Arsenal walifuta machozi kupitia kwa Torreira

0 comments:

Post a Comment