Ushirikianohuuwamuda mrefu utaifanya kampuni ya QNET kuendelea kuwa Muuzaji rasmi wa moja kwa moja wa timu ya wanawake na wanaume ya Manchester city.
Ushirikiano huu unaashiria hatua kubwa sana katika mwezi Mei mwaka 2018 wakati klabu ya Manchester city ilipoikaribisha kampuni ya QNET kama mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeves) katika Ligi ya Wanawake ya Super League.
Katika kipindi chote kijacho cha ushirikiano huu kampuni ya QNET itaendelea kutoa kliniki za mpira wa miguu zinazosimamiwa na klabu ya mpira a miguuya Manchester city kwajamii duniani kote, pamoja na kujihusisha na watumiaji na wasambazaji kupitia uhusiano huu na klabu ya City.
Kusherehekea tangazo hili QNET imezindua toleo dogo la saa zamkononiinayojulikanakama ‘QNETCity Champions’ zinazoundwa na kuzalishwa na mafundi mashuhuri wa nchini Switzerland.
Makamu wa Raisi Mwandamizi wa ushirikiano wa City Football Group, bwana Damian Willoughby, alitoa maoni yake na kusema “Tunafuraha kutangaza kwamba QNET imekuwa mshirika wa hivi karibuni kuongeza muda wa ushirikiano na Manchester City katika makubaliano ya muda mrefu ambayo yatashuhudia tukisherehekea miaka kumi ya kufanya kazi kwa pamoja.
Ushirikiano huu uliweka historia pale QNET ilipokuwa mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeve) katika ligi ya wanawake ya Super League na tunafuraha kuingia katika ukurasa mwingine kwa pamoja”.
Mkurugenzi Mkuu wa QNET Bwana, Malou Caluza alisema: “Huu ni ushirikiano unaothaminiwa sana kwa QNET na Manchester City kwa sababu utendaji bora ni msingi wa chapa zote mbili. Sote tunamsukumo kuelekea katika mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii, ari na kujitolea.
Kupitia ushirikiano huu, tumeweza kuwa na fursa ya kuwapeleka watoto kutoka katika familia zenye kipato kidogo kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda manchester kwaajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa miguu na kozi ya lugha ya kiingereza, ambayo kweli imekuwa ni fursa nzuri sana ya kubadilisha maisha kwa watoto walio wengi.
Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia mashabiki wetu.”
0 comments:
Post a Comment