Tuesday, August 27, 2019


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amekuja kivingine baada ya kuondolewa jana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aussems ameamua kuja na malengo ambayo kwa sasa ni kuhakikisha wanafanya vema katika mashindano yote yanayiowakabili ikiwemo taji la FA.

Kauli hiyo imekuja kutokana na Simba kuondolewa kwenye mashindano hayo makubwa na UD Songo kwa sare ya bao 1-1, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa.

"Malengo yetu kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote kuanzia Ligi Kuu, kombe la FA na mingine ambayo tutashiriki, " amesema Aussems.

Simba imeondoshwa kwenye mashindano hayo kutokana na faida ya bao la ugenini ambapo katika mechi ya kwanza huko Msumbiji ililazimishwa suluhu ya 0-0.

0 comments:

Post a Comment