Friday, August 9, 2019



EVERTON imethibitisha kuinasa saini ya mshambuliaji wa kikosi cha Arsenal, Alex Iwobi.

Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Nigeria amesaini kandarasi ya miaka mitano.

Iwobi akiwa Arsenal ambayo alijiunga nayo msimu wa mwaka 2015 amecheza jumla ya michezo 149 akiwa na washika bunduki hao.

Ameanza akiwa kijana kuwa na makazi ndani ya Emirates na amefunga jumla ya mabao 15 huku akitengeneza nafasi za mabao 27.

Everton imesema:" Kwa sasa Iwobi amesaini kandarasi ya miaka mitano na tutakuwa naye mpaka mwaka 2024 Juni.

0 comments:

Post a Comment