Friday, August 9, 2019




MANCHESTER United imethibitisha kuwa nyota wao mpya Harry Maguire na kiungo wao fundi, Paul Pogba wataanza kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea.

Maguire amemalizana na Manchester United akitokea Leicester City kwa dau la pauni milioni 80 siku ya Jumatatu.

Pogba alikuwa anasumbuliwa na majeraha kwa sasa yupo fiti kuendelea kupambana ndani ya kikosi hicho, 
Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa Harry ni mchezaji makini ataongeza ushindani ndani ya kikosi hicho.


 "Ni mrefu na mwili wake una nguvu kama ambavyo inatakiwa, amekuja ndani ya kikosi wakati sahihi, atakuwa na matokeo kwa Vijana. 

"Yupo tayari kucheza na nina uhakika nitaanza naye ndani ya kikosi sina mashaka naye kwa kuwa nimeongea naye,". 

United imeshinda jumla ya michezo yake sita kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya unaoanza leo waliyocheza wakati wa maandalizi.

0 comments:

Post a Comment