Wednesday, August 7, 2019


PAMBANO la marudiano kati ya Anthony Joshua na Andy Ruiz Jr linakaribia, baada ya promota Eddie Hearn kusema wapo katika hatua za mwishoni za makubaliano.
"Ninafahamu, nafikiria pambano litakuwa wapi, lakini inabidi nisubiri mikataba fulani ikamilike kisha tutatangaza,"alisema Hearn.
Hearn amesema kwamba Cardiff inabaki kuwa sehemu inayopewa kipaumbele kufanyika pambano hilo la marudiano, ingawa kuna sehemu nyingine mbili au tatu zinatajwa pia.
AJ anatarajiwa kuzichapa tena na Mmexico baada ya kuchapwa kwenye pambano la kwanza ukumbi wa Madison Square Garden, New York nchini Marekani Juni 1, mwaka huu.

Joshua mwenye urefu wa futi sita alivuliwa mataji yake yote ya dunia ya uzito ya IBF, WBA na WBO baada ya kupigwa na Ruiz kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba.
Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza Joshua kupoteza baada ya kushinda mapambano yake yote 22 ya awali, 21 kwa knockout, wakati Ruiz mwenye urefu wa futi nne alishinda pambalo la 32 na 22 kwa KO, huku akiwa amepoteza pambano moja pia

0 comments:

Post a Comment