Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa anataka kufutwa kibarua cha kuendelea kuinoa timu hiyo.
Zahera ambaye hivi sasa yupo na kikosi nchini Botswana kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, amesema hakuna ukweli wowote uliopo dhidi ya taarifa hizo., taarifa imeeleza.
Hivi karibuni kumekuwa kukielezwa kuwa Zahera hana maelewano na baadhi ya mabosi wake wakati huohuo baadhi y mashabiki na wadau wa Yanga wakisema hawamhitahi tena.
Zahera ambaye ni raia wa Congo DR, amekuwa akihusishwa kuondoka na taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema wako kwenye mpango wa kuajiri Kocha mwingine.
0 comments:
Post a Comment