Habari hizo zimeanza kuenea asubuhi ya leo siku ya Jumatatu kufuatia kuwa na msimu mzuri wa mwaka 2018/19 kwa makocha hao.
Kwa
upande wake Klopp alifanikiwa kunyakuwa taji la Champions League akiwa
na Liverpool kwa kumfunga Tottenham katika jiji la Madrid baada ya
Mauricio Pochettino kuifikisha Spurs katika hatua hiyo ya fainali kwa
mara yake ya kwanza.
Wakati
kwa upande wa Guardiola ameiyongoza City kunyakuwa taji la Premier
League mara mbili mfululizo baada ya kuizidi Liverpool after kwa
kujivunia point 98.
Huku makocha hawa wawili Guardiola na Klopp wakitarajiwa kuzidi kupambana msimu huu kuwania taji hilo la Premier League.
Man
City na Liverpool pia wamewakilishwa katika kundi la magoli kipa bora,
Ederson na Alisson sambamba na Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen kwenye
listi hiyo.Liverpool imemuingiza pia mchezaji wake Virgil van Dijk akishindana na Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo katika kuwania kipengele cha uchezaji bora, inakumbukwa pia beki huyo aliwashinda nyota hao kwenye tuzo ya ‘UEFA Player of the Year’.
0 comments:
Post a Comment