PATRICK Aussems, ameshusha breki leo na kuwaacha wachezaji wake wapumzike kwa muda kabla ya kurejea kazini.
Simba leo wameanza mapumziko yao ambayo yatadumu mpaka Alhamisi na watarejea kwenye mazoezi yao kuendelea na programu maalumu.
Maandalizi ya sasa kwa Simba ni maalumu kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 17 uwanja wa Uhuru.
Mchezo wa kwanza Simba ilianza kwa kujikusanyia pointi tatu kwa kushinda mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru.
0 comments:
Post a Comment