Monday, September 2, 2019



MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kupoteza kwake mchezo mbele ya Ruvu Shooting ni sehemu ya maisha ya soka hivyo mashabiki wasiwe na mashaka.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa ameona mashabiki wengi wamepoteza matumaini ya kushinda na kusahau kwamba mpira una matokeo tofati na vile ambavyo wanafikiri.

"Mashabiki wanapaswa wajue kwamba mpira una matokeo ya kipekee hivyo ni wakati wa kutulia na kuangalia maisha ya mpira yanaendelea," amesema. 

Yanga imevunja rekodi yake ya msimu uliopita kwa mwaka 2018/19 ambapo walicheza jumla ya michezo 19 bila kupoteza ila msimu huu kete ya kwanza wamepoteza mbele ya Ruvu Shooting.

0 comments:

Post a Comment