Klabu ya AC Milan ya Italia imefikia maamuzi mazito ya kumfukuza kazi kocha wao mkuu Marco Giampaolo baada ya kuifundisha timu hiyo katika michezo saba pekee.
AC Milan wamefikia maamuzi hayo ya kumtimua kazini Giampaolo baada ya klabu yao kuendelea kuwa katika hali mbaya Serie A na kuwa katika mwenendo usioridhisha toka kocha huyo alipomrithi Gennaro Gattuso Juni mwaka huu.
Katika mechi 7 Marco Giampaolo alizoziongoza chini ya AC Milan katika Serie A ameshinda michezo mitatu na kupoteza minne huku timu ikiwa nafasi ya 13 kwa kuwa na point 9 lakini ni point 3 dhidi ya timu zilizopo katika nafasi za kushuka daraja.
Kocha wa zamani wa Fiorentina na Inter Milan Stefano Pioli anaripotiwa kuziba pengo Giampaolo na kuifunza AC Milan ambao ni mabingwa mara saba wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment