Inaripotiwa kuwa Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Okwi hajafunga goli hata moja tangu ajiunge na Klabu ya Al Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri.
Ikumbukwe Mshambuliaji huyo ana rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 207/18, msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao 15.
Hata hivyo hadi kufikia sasa katika Ligi ya Misri, Okwi amecheza mechi tatu za Ligi huku mechi mbili dhidi ya Zamalek na El Gouna akicheza kwa dakika zote tisini, huku dhidi ya Al Masry akiingia dakika ya 65.
0 comments:
Post a Comment