Uongozi wa Azam FC umesema kuwa umempa ruhusa kocha wao, Etienne Ndayiragije kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania ili kuendelea pale alipoishia.
Ndayiragije leo amekwenda uwanja wa Chamazi ambapo timu yake ya zamani ilikuwa ikifanya mazoezi kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wake dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 23 uwanja wa Uhuru ikiwa chini ya kocha mpya Aristica Cioaba.
Ndayiragije amesema: "Leo nimekuja kuwaaga wachezaji wangu wa Azam FC na kumpa mikoba ya ukocha wangu kocha mpya kwa kuwa nimepewa majukumu mapya ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' nashukuru kwa sapoti na ushirikiano ambao nimekuwa nikipewa kwa muda wote niliokuwa ndani ya Azam FC,".
Maganga amesema kuwa wanafurahi kuona kocha wao akipewa majukumu mapya na mazito kwenye Taifa.
"Tumempa ruhusu kiroho safi akaitumikie muda wote timu ya Taifa vizuri tofauti na mwanzo ambapo alikuwa anatumikia timu mbili kwa wakati mmoja," amesema Maganga.
Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa mpango wa Kocha Mkuu bado upo atatangazwa muda wowote.
"Kesho tunakutana na Ndayiragije atukabidhi ripoti ya michuano ya Chan kisha tutafanya majadiliano naye kabla ya kuacha masuala yake kwenye benchi la ufundi kwani wengi wametuma maombi kuomba nafasi ya kuinoa timu," amesema
0 comments:
Post a Comment