Kiungo
wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, ameacha
azma yake ya kuhamia Manchester United mwezi Januari kwasababu
Wacroasia hawataki ahamie Manchester. (Mail)Unaweza pia kusoma:
La Liga imependekeza kwa shirikisho la soka la
Uhispania kwamba shindano la El Clasico lililiyopangwa tarehe 26
Oktoba Barcelona lifanyike badala yake tarehe 7 Disemba . Tayari
shirikisho hilo la mpira wa miguu limeomba kubadilisha gemu hiyo
ifanyike Madrid kutokana na hofu ya ghasia za kiraia.(AS)Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland analengwa na Manchester City. Kijana huyo Mnorway mwenye umri wa miaka 19 ni mtoto wa kiungo wa kati wa Manchester City Alf-Inge Haaland. (Sun)

Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 22 kutoka AC Milan mwezi Januari . (La Gazzetta dello Sport via Calciomercato)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, "si mzuri vya kutosha " kwa Bayern Munich, anasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Lothar Matthaus. (Sport 1, via Standard)
Tottenham watalenga kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Madrid Muhispania Isco,mwenye umri wa miaka 27, kama wataamua kumuuza Eriksen ifikapo mwezi Januari (El Desmarque - in Spanish)
Mlindalango wa Liverpool Mhispania Adrian, mwenye umri wa miaka 32, anasema the Reds walimkanyaga mara mbili na kumuumiza mlindalango wa Brazil Alisson Becker,mwenye umri wa miaka 27. (Telegraph)
Watfordwamekataa ombi kutoka kwa Fluminense la kuendelea kubaki na Joao Pedro nchini Brazil hadi Juni -2020. Hornets wamekubali kusiani mkataba na kijana huyo mchanga mwenye umri wa miaka 18 tu anayecheza safu ya mashambulizi Januari 1 . (Watford Observer)
Liverpool ina matumaini ya kuipiku Chelsea kwa kusiani mkataba na mchezaji wa kimataifa wa vijana wadogo ya England kutoka Exeter anayecheza safu ya kati Ben Chrisene ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15. (Sun)
0 comments:
Post a Comment