Bingwa mara 20 wa Grand Slam, Roger Federer amerudi kwenye michuano ya Roland Garros mwaka 2019 baada ya kupotea kwa miaka mitatu, hata hivyo mambo hayakuwa mazuri kwani lifungwa na Rafael Nadal katika nusu fainali.
Mchezaji huyo kutoka Uswizi mwenye miaka 38, ambaye ameshinda Michuano ya Wazi ya Ufaransa Mara moja tu, mwaka 2009, pia atapambana mwaka ujao kwenye Olimpiki ya Tokyo.
Federer, analenga kuongeza medali ya dhahabu kwa mchezaji mmoja mmoja huko Tokyo baada ya kufungwa na Andy Murray kwenye Olimpiki ya London mwaka 2012.
Federer, aliyemshinda Albert Ramos-Vinolas katika hatua ya fainali ya Shanghai Masters, ameshafuzu kucheza fainali za ATP huko London mwezi Novemba
0 comments:
Post a Comment