Friday, October 18, 2019


Klabu ya Inter Milan ipo katika mipango ya kumsajili kiungo wa Manchester United, Nemanja Matic mwenye umri wa miaka 31, katika dirisha lijalo la mwezi Januari. (Sun)
Nemanja Matic anatafutwa na Inter Mila
Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland analengwa na Manchester City. Kijana huyo Mnorway mwenye umri wa miaka 19 ni mtoto wa kiungo wa kati wa Manchester City Alf-Inge Haaland. (Sun)
Erling Haaland analengwa na Manchester City
Mchezaji wa safu ya ushambuliaji wa klabu ya Lyon, Moussa Dembele anataka kurejea ligi kuu England , huku akiripotiwa kusakwa na Everton na Manchester United.
Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England
Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 22 kutoka AC Milan mwezi Januari . (La Gazzetta dello Sport via Calciomercato)
Tottenham na Manchester United ni miongoni mwa klabu kadhaa zilizowasiliana na Borussia Monchengladbach kuhusiana na namna wanavyoweza kumpata Mswiss anayecheza safu ya kati Denis Zakaria ambaye sasa ana umri wa miaka 22. (Bild – in German)
Tottenham watalenga kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Madrid Muhispania Isco, mwenye umri wa miaka 27, kama wataamua kumuuza Eriksen ifikapo mwezi Januari (El Desmarque – in Spanish)
Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, mwishoni mwa msimu ikiwa atbakia kuwa mchezaji wa ziada. (Football Insider)
Mlindalango wa Liverpool Mhispania Adrian, mwenye umri wa miaka 32, anasema the Reds walimkanyaga mara mbili na kumuumiza mlindalango wa Brazil Alisson Becker,mwenye umri wa miaka 27. (Telegraph)
Watfordwamekataa ombi kutoka kwa Fluminense la kuendelea kubaki na Joao Pedro nchini Brazil hadi Juni -2020. Hornets wamekubali kusiani mkataba na kijana huyo mchanga mwenye umri wa miaka 18 tu anayecheza safu ya mashambulizi Januari 1 . (Watford Observer)
Winga wa Crystal Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, hutoa 10% ya mshahara wake kama msaada katika nchini Ivory Coast ambako ndio asili yake , ikiwa ni ni pamoja na kusaidia kituo cha yatima kinachoendeshwa na dada yake. (Mirror)
Liverpool ina matumaini ya kuipiku Chelsea kwa kusiani mkataba na mchezaji wa kimataifa wa vijana wadogo ya England kutoka Exeter anayecheza safu ya kati Ben Chrisene ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15. (Sun)

0 comments:

Post a Comment