Ripoti kutoka vyombo vya habari Hispania zinasema kuwa huwenda Jumatatu ya wiki ijayo ndiyo ikafahamika hatma ya mchezo huo mkubwa unao fuatiliwa na wapenzi wengi wa soka dunia baada ya kughairishwa kufanyika Camp Nou tarehe 26 Oktoba.
Hapo awali ilitarajiwa maamuzi ya ‘game’ hiyo yangefanyika leo siku ya Ijumaa lakini limeshindikana na kupelekwa hadi Jumatatu kwa mujibu wa Marca.
Ukubwa wa mchezo huo unatokana hasa na miamba hiyo miwili ya soka Barcelona na Real Madrid kutoka katika majimbo mawili tofauti nchini Hispania, lakini pia ikichagizwa na maswala ya kisiasa pamoja na ubora wa wachezaji wanao sajiliwa.
El Clasico ilikusudiwa kufanyika Barcelona lakini kutokana na changamoto hizo za maandamano Catalunya inatarajiwa sasa ‘game’ hiyo huwenda ikahamishiwa katika jiji la Madrid.
Hata hivyo maamuzi hayo bado yanaonekana kusuasua kwa pande zote mbili Barcelona na hata Real Madrid hivyo Jumatatu ijayo ndiyo siku pekee itakayofahamika hatma yake.
‘Game’ hiyo ambayo huwenda ikapangwa kufanyika Desemba 18, lakini kwa upande wa La Liga haitaki upigwa tarehe hiyo kwakuwa itaangukia siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment