Friday, October 18, 2019

 

Timu ya Al Ahly imetuma taarifa rasmi kwa Chama cha soka cha Misri (EFA), ikiwaambia kuwa hawatocheza michezo yoyote ya Ligi kufatia kuahirishwa kwa Derby ya Cairo.

Al Ahly walipangwa kuwakaribisha wapinzani wao Zamalek siku ya Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri. Lakini EFA iliamua kuahirisha mchezo huo hadi tarehe isiyojulikana, kutokana na masuala ya usalama wa nchi hiyo.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na kituo cha habari cha Al Ahly, Klabu hiyo imetuma taarifa rasmi kwa EFA ikiwajulisha kuwa hawatocheza michezo yoyote ijayo ya Ligi Kuu ya Misri hadi watakapoikabili Zamalek.

Msimamo wa ligi kuu ya Misri (2019-20)
1. Al Ahyl, Pts 9
2. Pyramids, Pts 8
3. El Mokawloon

0 comments:

Post a Comment