Wednesday, October 23, 2019



LEO uwanja wa Taifa Simba na Azam zitakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu.

Wachezaji wanne wataukosa mchezo huu kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwa Simba nyota hawa watakosekana leo John Bocco ameanza mazoezi mepesi ila leo hatacheza kwa kuwa hayupo fiti.

Jonas Mkude na Mohamed Hussein 'Tshabalala' wanatibu majeraha waliyoyapata kwenye timu ya Taifa.

Kocha Mkuu wa Simba, Patric Aussems amesema kuwa atatafuta mbadala wao kwani ana kikosi kipana.

Kwa upande wa Azam FC wao hawana majeruhi kabisa isipokuwa ni maamuzi ya Kocha kuamua kumtumia nahodha Agrey Moris ambaye ametoka kupona majeraha yake muda si mrefu.

0 comments:

Post a Comment