Saturday, October 5, 2019



Hali ya mambo huenda isiwe poa tena kwa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkode kutokana na tukio analodaiwa kulifanya hivi karibuni wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kwenda Kanda ya Ziwa kucheza mechi za Ligi Kuu Bara.

Mkude hakusafiri na timu hiyo baada ya kudaiwa kuachwa na ndege ikielezwa alipitiwa na usingizi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi.

Hata hivyo, habari ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka ndani ya Simba zimedai kilichosababisha Mkude aachwe ni pombe kwani alienda nyumbani na kila alipokuwa akipigiwa simu akawa hapokei.

“Kwa hiyo kesho (leo) uongozi utaweka wazi hatua ambazo utamchukulia kutokana na kosa hilo alilofanya ambalo kusema kweli si la kiungwana,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Suala lake kwa sasa lipo kwa uongozi wa juu na siyo kwa kocha tena kwani, kocha yeye anataka nidhamu katika kikosi chake na ameshatoa msimamo wake kwa uongozi kuhusiana na Mkude, hivyo kesho (jana) ndiyo tutajua hatima yake.”

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems alisema: “Suala hilo kwa sasa siwezi kulizungumzia watafuteni viongozi wa klabu.”

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingiza ili aweze kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokewa. Alipotafutwa Mkude na kuulizwa juu ya madai hayo alisema:

“Watu wanaishi kwa kukariri, siwezi kuacha kwenda Kagera kisa pombe, nina maisha yangu binafsi. Nitafuta baadaye tutazungumza kuhusu hilo vizuri.

0 comments:

Post a Comment