Saturday, October 5, 2019


Hapo jana kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara kulikuwa na mchezo mkali na wa aina yake katika uwanja wa Uhuru, wakati Yanga SC ilipokuwa ikiwakabili timu ya Polisi Tanzania.
Image
Kwenye mchezo huo ulishudiwa ukimalizika kwa sare ya mabao 3 – 3, huku mshambuliaji nyota wa Polisi Tanzania, Ditram Nchimbi akifanikiwa kuondoka na mpira baada ya kufungua mabao matatu peke yake ‘Hat-trick’.
Kufuatia uwezo mkubwa aliyouonyesha Nchimbi kunako ligi kuu, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ndairagije Ettiene ameamua kumuongeza nyota huyo katika kikosi chake na hivyo sasa kufikisha idadi ya wachezaji 29

0 comments:

Post a Comment