BEKI
wa kati wa Azam FC, Oscar Masai, ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya
Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilichoingia kambini jana.
Stars
imeingia kambini kujiandaa na mechi mbili, ya kwanza ikiwa ni ya
kirafiki na Rwanda 'Amavubi', itakayopigwa jijini Kigali Oktoba 14 mwaka
huu, pamoja na ile ya marudiano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika
kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Sudan Oktoba 18 mwaka huu.
Masai, ambaye ni mmoja wa mabeki chipukizi wanaochipukia kwa kasi
nchini, alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana 'Ngorongoro
Heroes' kilichotwaa ubingwa wa vijana wa CECAFA wikiendi iliyopita.
Wachezaji wengine wa Azam FC walioitwa kikosi hicho ni Nahodha Msaidizi,
Frank Domayo 'Chumvi', Mudathir Yahya, Salum Abubakar 'Sure Boy', Idd
Seleman 'Nado' na mshambuliaji Shaaban Chilunda.
0 comments:
Post a Comment