MESSI AFIKISHA MABAO 113 LIGI YA MABINGWA BACRA IKISHINDA 2-1
Mshambuliaji
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Barcelona
dakika ya tatu katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Slavia Prague
kwenye mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja
wa Sinobo mjini Prague. Bao lingine la Barcelona lilifungwa na Peter
Olayinka aliyejifunga dakika ya 57, wakati la Slavia Prague lilifungwa
na Jan Boril dakika ya 50 na Messi sasa amefikisha mabao 113 ya kufunga
kwenye Ligi ya Mabingwa sasa akimfuatia Cristiano Ronaldo anayeongoza
kwa mabao yake 127
0 comments:
Post a Comment