Friday, October 25, 2019



MSANII aliyekuwa akimilikiwa na Lebo ya WCB, Harmonize amesema kuwa amelazimika kuuza nyumba zake tatu pamoja na mali zake nyingine kuilipa lebo yake hiyo ya zamani kiasi cha Tsh milioni 500 ili kuvunja mkataba nayo na kupata hakimiliki ya jina lake na kazi zake za sanaa.

Harmonize amesema hayo jana wakati akipiga stori na XXL ya Clouds FM kwenye media tour ambayo anaitangaza ngoma yake mpya ya UNO.

“Ukweli hatupo sawa na uongozi uliopita, sitaki kusema uongo, mahusiano yangu na uongozi uliopita sio kama zamani.

Naomba niwashukuru  kwa sababu wao ndo wamesababisha mimi kuwa hapa! Japokuwa kuna matatizo ya ndani ambayo siwezi kuyasema hadharani nimeamua kufanya kazi kama msanii huru lakini sipendi kuwavunjia heshima.

“Mkataba wangu ulikuwa unanitaka nilipe shilingi milioni 500 kama nikiondoka ili niweze kupata hakimiliki ya jina langu pamoja na nyimbo zangu. Hivyo sikuwa na hela kabisa. Nimeuza nyumba zangu tatu na baadhi ya mali, deni limebaki kidogo.

“Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli aliwahi kunipigia simu saa 10 usiku, akaniambia ‘wimbo wako (Kwangwaru Remix) unajenga nchi kwani umewaonesha watu maendeleo’. Pia alisema anapenda wimbo wangu wa ‘Matatizo’ akampa simu Mama Janeth nikazungumza naye.

Rais alisema Mama Janeth ni shabiki yangu. Naomba nimshukuru kwa dhati kabisa Mheshimiwa John Pombe Magufuli.

“Unaambiwa ‘wish’ ya Rais ni oda na mimi kama Mtanzania siwezi kukataa naamini watu wa Tandahimba wamelipokea na mimi nimelipokea kwa hiyo sisi tunalifanyia kazi.

“Ni kitu ambacho kinamaliza wasanii wengi, na ukiangalia wamiliki wa media ni walewale, natamani migogoro ya media iishe, chanzo ni biashara lakini tukizungumza itaisha tu. Kuhusu wao kushindwa kuhudhuria ndoa yangu, niliweka nadhiri kuwa siku ya ndoa ningependa wahudhuriaji wawe ni ndugu zangu.

“Kwenye album yangu nimefanya na Jidenna, Cassanova na Morgan Heritage. Nilitamani kuachia album yangu mwisho wa mwaka huu, itakuwa ni ya kuunganisha muziki na wasanii wa Afrika Mashariki pamoja na Magharibi.

Kuna colabo za wasanii toka pande zote hizo. Nitaiachia mwakani. UNO nimeandika katika wakati ambao nina wakati mgumu, na nimefanya ili ku-prove watu kwamba I can do it.

“Hawa ‘Security’ unaowaona ni kaka zangu ambao mimi wakati niko Rajabu nahangaika mtaani tumehangaika wote imefikia wakati Mwenyezi Mungu amenipa mimi nafasi kidogo naona sasa kwa nini nisiwasogeze kaka zangu tukipata tonge tunagawana?”

"Mimi ni Harmonize lakini nyuma ya Harmonize kuna Rajabu! Kwenye mambo ya kibinadamu Rajabu lazima ahusike ndio maana nilishiriki kwenye mazishi ya Ruge! Nilichokifanya hakikuniletea matatizo kwenye uongozi wangu uliopita,” amesema Harmonize.

0 comments:

Post a Comment