Friday, October 25, 2019



Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameingiwa na hofu kuhusiana na kuumia kwa wachezaji wake wawili Sadney Urikhob pamoja na Maybin Kalengo.

Urikhob aliumia katika mechi ya ligi dhidi ya Mbao FC wakati Kalengo akiumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba SC.

Imeelezwa kuwa Zahera amesema kukosekana kwa wawili hao katika mechi dhidi ya Pyramids kwa namna moja ama nyingine kunaweza kukawa na pengo kwao.

Amemtaja pia David Molinga ambaye ataikosa mchezo huo kuwa nayo itapunguza nguvu ndani ya timu sababu bado hajapata kibali cha kuitumikia Yanga kwenye mashindano hayo.

Hata hivyo, Zahera ameeleza atapambana kwa kutumia wachezaji walionao ili waweze kupata ushindi katika mechi hiyo muhimu kwa Yanga.

0 comments:

Post a Comment