KIKOSI cha Yanga juzi kimelamba kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni baada ya ushindi walioupata dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza. Yanga iliibuka na ushindi dhidi ya Mbao kwa kufunga bao 1-0 hivyo kujikuta ikiwa na pointi saba,nafasi ya tano.
Wadhamini wa Yanga GSM wamekuwa na utaratibu wa kuwazawadi fedha wachezaji wa timu hiyo pindi wanapofanya vizuri ambapo wameanza katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa hivi karibuni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo waliwapatia kiasi cha shilingi milioni 10. A
kizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rogers Gumbo amesema kuwa, GSM wamewapatia kiasi cha shilingi milioni 10 wachezaji wa Yanga baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Mbao FC ikiwa ni muendelezo wa ahadi yao.
“GSM wamewapatia shilingi milioni 10 wachezaji wa Yanga kama motisha baada ya ushindi dhidi ya Mbao kwa kuibuka na pointi tatu muhimu, huu ni muendelezo baada ya kutoa katika mchezo dhidi ya Coastal Union.
“Kuhusu mechi yetu na Pyramids bado hatujaandaa mchakato wa kuwapatia ahadi wachezaji kwa kuwa bado mapema ila muda ukikaribia lazima tuwape ahadi,” alisema Rogers.
0 comments:
Post a Comment