WAKIJIANDAA kuwavaa wapinzani wao Pyramids FC, Nahodha na kiungo fundi wa Yanga Mkongomani, Papy Tshishimbi ana matumaini ya ushindi katika mchezo huo baada ya kumaliza tatizo walilokuwa nalo awali.
Tshishimbi alisema katika michezo iliyopita ya ligi na michuano ya kimataifa walikuwa wanashindwa kupata matokeo ya ushindi kutokana na tatizo la safu ya ushambuliaji ambalo tayari wamepata tiba yake.
Tshishimbi alisema hilo limeonekana kwenye mchezo wao wa ligi na Mbao ambao walitengeneza nafasi mbili pekee kati ya hizo wakafanikiwa kufunga moja bao lililofungwa na Saidney Urikhob.
Aliongeza kuwa ushindi huo walioupata umedhihirisha tatizo hilo la ufungaji limeanza kumalizika huku akiwa na imani kubwa ya kuwafunga Pyramids hapa nyumbani.
“Timu yetu imekuwa na tatizo la ufungaji tangu kuanza kwa msimu huu kwa kuanzia michuano ya kimataifa na ligi ambalo hivi sasa ninaona linaanza kumalizika taratibu baada ya kocha kulifanyia kazi.
“Mfano katika mchezo wetu na Mbao tulitengeneza nafasi mbili pekee za kufunga mabao lakini kati ya hizo moja tukafunga na nyingine mimi nikikosa bao kwa kichwa nilichokipiga na kugonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani kabla ya kuokolewa na mabeki.
“Hiyo inanipa picha halisi kuwa tutapata ushindi wa hapa nyumbani wa Kombe la Shirikisho mara tutakapocheza na Pyramids hapa nyumbani, kikubwa tunachotakiwa kukifanya ni kutumia kila nafasi vizuri katika kufunga
0 comments:
Post a Comment