Simba
SC baada ya kuwa na msimu mzuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu
2018/19 kiasi cha kufika robo fainali, muwekezaji wa timu hiyo MO Dewji
alitangaza kuwa wamempa kocha wao Patrick Aussems malengo ya
kufikia.Simba SC ilidaiwa kumpa target kuwa msimu huu wa 2019/20
anatakiwa afike nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa
bahati mbaya Simba SC ikatolewa na UD Songo round ya awali, vipi hatma
ya kocha Aussems wataendelea nae tena au anatafutiwa mbadala? CEO wa
Simba SC Senzo Mazingiza amefunguka kupitia AyoTV.
“Hadi
sasa Mr Patrick Aussems ni kocha wa Simba SC anaendelea kufanya kazi
yake kuna vitu vingi msimu uliopita na sasa tunafanyaje sasa tukirudi
nyuma (kumuondoa) tunaharibu kila kitu kwa sababu hatujafikia malengo
yetu? tunatakiwa kutafuta njia ya kuhakikisha klabu inakuwa imara na
inacheza vizuri ila hadi sasa Patrick Aussems anaendelea kuwa kocha wa
Simba”
0 comments:
Post a Comment