Kiungo wa PSG, Neymar ametupwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia nyama za paja akiwa na timu ya Taifa ya Brazil.
Brazil walikuwa wanavaana na Nigeria kwenye mchezo wa kirafi ki wakati mchezaji huyo alipoumia na kutolewa uwanjani kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare.
Hili ni pigo kubwa kwa PSG ambayo msimu huu ilikuwa imeshaanza kuweka matumaini makubwa kwake kwa kuwa alishaanza msimu vizuri.
Hata hivyo, daktari wa timu ya Taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar, amesema kuwa majeraha ya mchezaji huyo siyo makali sana.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alipelekwa moja kwa moja kwa daktari wake wa timu yake ya PSG. Juzi aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram, akiwa kitandani huku akiwa amefunga bandeji ngumu.
0 comments:
Post a Comment