Aguero ambaye hakuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichokusanyika kucheza michezo ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA, alikuwa njiani na gari lake anaelekea mazoezini lakini kwa bahati nzuri hakuumia wala kupata majeraha yoyote na alienda kuendelea na mazoezi kama kawaida.
Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Sergio Kun Aguero kupata ajali ya gari aliwahi kupata 2017 akiwa Amsterdem Uholanzi alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kuangalia show ya msanii wa Argentina Maluna aliyekuwa anafanya tamasha nchini Uholanzi, wakati Aguero anarudi na kuelekea Aiport ndio taxi aliyokuwa amepanda ikaacha njia na kugonga nguzo.
0 comments:
Post a Comment