Thursday, October 17, 2019



Idara ya Usimamizi wa ligi kuu ya soka ya nchini Hispania La Liga imeomba mechi watani wa kihistoria kwenye ligi hiyo (El Clasico) inayotarajiwa kupigwa mnamo Oktoba 26 ibadilishiwe uwanja kutoka uwanja wa Barcelona wa Nou Camp kwenda uwanja wa Real Madrid wa Bernabeu kutokana na hofu ya kutokea machafuko kufuatia hali tete inayoendelea kwa siku kadhaa sasa ikijumuisha maandamo makubwa na migomo .
Kumekuwa na siku za maandamano huko Barcelona baada ya viongozi tisa wa kujitenga wa Kikatalani kufungwa jela Jumatatu .
La Liga imetuma ombi hilo kwa Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF), na vilabu vyote viwili vimeshauriwa kutoa maoni pia kuhusu mtazamo huo wa Laliga .
Lakini kwa mujibu wa medani mbalimbali za uchambuzi wa masuala ya michezo, historia inaeleza kuwa Barcelona haijawahi kukubaliana na maombi kama hayo ikiwahi kusema kubadili sio lazima .
Maandamano zaidi yanatarajiwa jijini siku ya mechi, hivyo ombi hilo linakuja kwa sababu ya mazingira ya kipekee yaliyo zaidi ya uwezo wa Laliga.

0 comments:

Post a Comment