Thursday, October 17, 2019


Kipa wa Manchester United, David De Gea akiugulia maumivu baada ya kuumia jana akiichezea timu yake ya taifa, Hispania ikitoa sare ya 1-1 na Sweden katika mchezo wa Kundi F kufuzu Euro 2020 Uwanja wa Friends Arena mjini Solna.
De Gea alitolewa dakika ya 60 nafasi yake ikichukuliwa na Kepa Revuelta na sasa yuko hatarini kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool Jumapili Uwanja wa Old Trafford. Katika mchezo wa jana, Marcus Berg alianza kuifungia Sweden dakika ya 50, kabla ya Rodrigo kuisawazishia Hispania dakika ya 90 na ushei

0 comments:

Post a Comment